Mstari wa Siku

[Copy and send, from here:]

Mstari wa Siku:

Habari za asubuhi! 🙂

https://www.wordproject.org/bibles/votd3/index_sw.htm


Mistari ya kila mwezi ya Biblia:

Day 1
"Bwana asipoijenga nyumba Waijengao wafanya kazi bure. Bwana asipoulinda mji Yeye aulindaye akesha bure.
- Zaburi 127:1

Day 2
"Bwana ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa Bwana Na kumngojea kwa utulivu.
- Maombolezo 3:25-26

Day 3
"Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. -
- Warumi 8:28

Day 4
"Mwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.
- Zaburi 4:4

Day 5
"Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni..
- Yohana 16:21

Day 6
"Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. -
- Waefeso 2:8

Day 7
" Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
- Warumi 13:8

Day 8
"Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. -
- Zaburi 68:19

Day 9
"bali wao wamngojeao Bwana watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
- Isaya 40:31

Day 10
"Mbingu na nchi zitapita; lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
- Mathayo 24:35

Day 11
"Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji.
- Mithali 11:24

Day 12
"Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo.
- Yohana 13:34

Day 13
"Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mapokeo ya wanadamu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, wala si kwa jinsi ya Kristo.
- Wakolosai 2:8

Day 14
"Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu.
- 2 Wakorintho 2:14

Day 15
"Kwa kuwa Wewe Bwana ndiwe kimbilio langu; Umemfanya Aliye juu kuwa makao yako. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
- Zaburi 91:9, 10

Day 16
"Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
- Warumi12:17

Day 17
"Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo.
- Mwanzo 1:24

Day 18
"Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi.
- Isaya 35:4

Day 19
"Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana; tusiviangalie vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele.
- 2 Wakorintho 4:17-18

Day 20
"Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
- Yakobo 3:18

Day 21
"Je! Huyo aliyenifanya mimi ndani ya tumbo, siye aliyemfanya na yeye? Si yeye mmoja aliyetufinyanga tumboni?
- Ayubu 31:15

Day 22
"Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake.
- Waebrania 13:15

Day 23
"Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana.
- Yeremia 1:8

Day 24
"Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
- Yohana 17:24

Day 25
"Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana,
- Zaburi 91:5

Day 26
"Mtu mmoja miongoni mwenu atafukuza watu elfu; maana Bwana, Mungu wenu, ndiye anayewapigania, kama alivyowaambia.
- Yoshua 23:10

Day 27
"Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
- Warumi5:1

Day 28
"Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria, Hata sala yake ni chukizo.
- Mithali 28:9

Day 29
" Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli.
- Yohana 17:17

Day 30
"Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu. Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
- 1 Wakorintho 3:6, 7

Day 31
"Baba yangu na mama yangu wameniacha, Bali Bwana atanikaribisha kwake.
- Zaburi 27:10