Amani

0:00
0:00

  • Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
    Mwanzo 15:15
  • Bwana atawapa watu wake nguvu; Bwana atawabariki watu wake kwa amani.
    Zaburi 29:11
  • Uache mabaya ukatende mema, Utafute amani ukaifuatie.
    Zaburi 34:14
  • Bali wenye upole watairithi nchi, Watajifurahisha kwa wingi wa amani.
    Zaburi 37:11
  • Umwangalie sana mtu mkamilifu, Umtazame mtu mnyofu, Maana mwisho wake mtu huyo ni amani.
    Zaburi 37:37
  • Wana amani nyingi waipendao sheria yako, Wala hawana la kuwakwaza.
    Zaburi 119:165
  • Mimi ni wa amani; Bali ninenapo, wao huelekea vita.
    Zaburi 120:7
  • Njia za mtu zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye.
    Mithali 16:7
  • Wakati wa kupenda, na wakati wa kuchukia; Wakati wa vita, na wakati wa amani.
    Mhubiri 3:8
  • Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
    Isaya 9:6
  • Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.
    Isaya 26:3
  • Na kazi ya haki itakuwa amani; na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima.
    Isaya 32:17
  • Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.
    Isaya 54:13
  • Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.
    Isaya 55:12
  • Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu.
    Isaya 57:21
  • Njia ya amani hawaijui; wala hapana hukumu ya haki katika miendo yao; wamejifanyizia njia zilizopotoka; kila apitaye katika njia hizo hajui amani.
    Isaya 59:8
  • Wameiponya jeraha ya watu wangu kwa juu juu tu, wakisema, Amani, Amani, wala hapana amani.
    Yeremia 6:14
  • Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
    Yeremia 29:11
  • Tazama, nitauletea afya na kupona, nami nitawaponya; nami nitawafunulia wingi wa amani na kweli.
    Yeremia 33:6
  • Uharibifu unakuja; nao watatafuta amani, lakini haitapatikana.
    Ezekieli 7:25
  • yaani, manabii wa Israeli, watabirio habari za Yerusalemu, na kuona maono ya amani katika habari zake; wala hapana amani, asema Bwana MUNGU.
    Ezekieli 13:16
  • Na kwa mashauri yake atafanikisha hila mkononi mwake; naye atajitukuza nafsi yake moyoni mwake; naye atawaangamiza wengi katika hali yao ya salama; naye atasimama kushindana naye aliye Mkuu wa wakuu; lakini atavunjika, bila kazi ya mikono.
    Danieli 8:25
  • Wakati wa amani atapaingia mahali palipofanikiwa sana pa wilaya hiyo; naye atatenda mambo ambayo baba zake hawakuyatenda, wala babu zake; atatawanya kati yao mawindo, na mateka, na mali; naam, atatunga hila zake juu ya ngome, hata wakati ulioamriwa.
    Danieli 11:24
  • Tazama, juu ya milima iko miguu yake aletaye habari njema, atangazaye amani. Zishike sikukuu zako, Ee Yuda, uziondoe nadhiri zako; kwa maana yule asiyefaa kitu hatapita kati yako tena kamwe; amekwisha kukatiliwa mbali.
    Nahum 1:15
  • Agano langu naye lilikuwa agano la uhai na amani; nami nikampa ili aogope, naye akaniogopa, akalicha jina langu.
    Malaki 2:5
  • Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
    Mathayo 5:9
  • Na nyumba ile ikistahili, amani yenu na iifikilie; la, kwamba haistahili, amani yenu na iwarudie ninyi.
    Mathayo 10:13
  • Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta amani duniani; la! Sikuja kuleta amani, bali upanga.
    Mathayo 10:34
  • Akaamka, akaukemea upepo, akaiambia bahari, Nyamaza, utulie. Upepo ukakoma, kukawa shwari kuu.
    Marko 4:39
  • Akamwambia, Binti, imani yako imekuponya, enenda zako kwa amani, uwe mzima, usiwe na msiba wako tena.
    Marko 5:34
  • Chumvi ni njema; lakini chumvi ikiwa si chumvi tena, mtaitia nini ikolee? Mwe na chumvi ndani yenu, mkakae kwa amani ninyi kwa ninyi.
    Marko 9:50
  • Kuwaangaza wakaao katika giza na uvuli wa mauti, Na kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.
    Luka 1:79
  • Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia.
    Luka 2:14
  • Akamwambia yule mwanamke, Imani yako imekuokoa, enenda zako kwa amani.
    Luka 7:50
  • Na nyumba yo yote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu;
    Luka 10:5
  • Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali.
    Luka 14:32
  • wakasema, Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana; amani mbinguni, na utukufu huko juu.
    Luka 19:38
  • Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu.
    Luka 24:36
  • Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
    Yohana 14:27
  • Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
    Yohana 16:33
  • kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watakatifu. Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
    Warumi 1:7
  • Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Wala njia ya amani hawakuijua. Kumcha Mungu hakupo machoni pao.
    Warumi 3:16-18
  • Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo,
    Warumi 5:1
  • Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.
    Warumi 8:6
  • Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
    Warumi 10:15
  • Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
    Warumi 12:18
  • Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
    Warumi 14:17
  • Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.
    Warumi 14:19
  • Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
    Warumi 15:13
  • Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.
    Warumi 15:33
  • Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
    1 Wakorintho 1:3
  • Lakini Mungu ametuita katika amani.
    1 Wakorintho 7:15
  • Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani; vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu.
    1 Wakorintho 14:33
  • Hatimaye, ndugu, kwaherini; mtimilike, mfarijike, nieni mamoja, mkae katika amani; na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
    2 Wakorintho 13:11
  • Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.
    Wagalatia 1:3
  • Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.
    Wagalatia 6:16
  • Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
    Wagalatia 5:22
  • Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani.
    Waefeso 2:14, 15
  • na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.
    Waefeso 4:3
  • na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani;
    Waefeso 6:15
  • Mambo mliyojifunza kwangu na kuyapokea, na kuyasikia na kuyaona kwangu, yatendeni hayo; na Mungu wa amani atakuwa pamoja nanyi.
    Wafilipi 4:9
  • na kwa yeye kuvipatanisha vitu vyote na nafsi yake akiisha kufanya amani kwa damu ya msalaba wake; kwa yeye, ikiwa ni vitu vilivyo juu ya nchi, au vilivyo mbinguni.
    Wakolosai 1:20
  • Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.
    Wakolosai 3:15
  • Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi.
    1 Wathesalonike 5:4
  • Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.
    2 Timotheo 2:22
  • Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
    Waebrania 12:14
  • Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu,
    Waebrania 13:20
  • Na tunda la haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
    Yakobo 3:18
  • Na aache mabaya, atende mema; Atafute amani, aifuate sana.
    1 Petro 3:11
  • Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda alipewa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.
    Ufunuo wa Yohana 6:4