Uchaguzi wa Mistari ya Biblia

Uchaguzi huu ni mwongozo, wenye mistari yote ya msingi juu ya masomo mbalimbali. Huu siyo mbadala wa kusoma Biblia yote, bali inatusaidia kukumbuka na kupata uhakika juu ya imani yetu. Ni matumaini yetu kuwa utatiwa moyo, utaimarishwa na kusaidiwa. Katika lugha nyingine utaweza kupata maandiko katika sauti yakiwa kwenye faili ya sauti na ukipakua faili kutoka kwenye tovuti, utaweze kusikiliza maandiko mara kwa mara bila kutumia mtandao. Hapa chini chagua mojawapo ya mada zifuatazo.