Mstari wa Siku

[Copy and send, from here:]

Mstari wa Siku:

Habari za asubuhi! 🙂

https://www.wordproject.org/bibles/votd/03/index_sw.htm


Mistari ya kila mwezi ya Biblia:


Machi 1
"Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.
- Yeremia 29:11


Machi 2
"..Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemchemi za maji.
- Ufunuo wa Yohana< 14:7

Machi 3
"Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana. Naam, vyote vilivyo ndani yangu Vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana, Wala usizisahau fadhili zake zote.
- Zaburi 103:1,2

Machi 4
"Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe.
- 2 Timotheo 2:13

Machi 5
"Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. ...
- 2 WAKORINTHO 12:9

Machi 6
"Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
- 1 Mambo ya Nyakati 16:34

Machi 7
"Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
- 1 Yohana 5:4

Machi 8
"Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa Bwana ananitegemeza.
- Zaburi 3:5

Machi 9
"..kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile.
- 2 Timotheo 1:12

Machi 10
"Thou shalt be hid from the scourge of the tongue: neither shalt thou be afraid of destruction when it cometh.
- Ayubu 5:21

Machi 11
"Bwana, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uisawazishe njia yako mbele ya uso wangu,
- Zaburi 5:8

Machi 12
"Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
- Zaburi 46:1

Machi 13
"Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo.
- 1 Wakorintho 13:13

Machi 14
"Pombeni bila kukoma;
- 1 Wathesalonike 5:17

Machi 15
"usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
- Isaya 41:10

Machi 16
"Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
- Warumi 1:28

Machi 17
"..akawapa amri juu ya pepo wachafu, wawatoe, na kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina.
- Mathayo 10:1

Machi 18
"Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
- Waebrania 4:16

Machi 19
"Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.
- Mwanzo 4:1

Machi 20
"Maana Kristo hakunituma ili nibatize, bali niihubiri Habari Njema; wala si kwa hekima ya maneno, msalaba wa Kristo usije ukabatilika.
- 1 Wakorintho 1:17

Machi 21
"Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao.
- Zaburi 86:5

Machi 22
"Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. -
- Yohana 3:3

Machi 23
".. Ikawa walipokuwa wakienda walitakasika.
- Luka 17:14

Machi 24
"Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye.
- Waebrania 10:38

Machi 25
"..Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini;..
- Isaya 30:15

Machi 26
"..kadiri mlivyomtendea mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi.
- Mathayo 25:40

Machi 27
"Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake; ..
- Malaki 4:2

Machi 28
"..Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
- Mathayo 4:4

Machi 29
"Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye Bwana atakuwa salama.
- Mithali 29:25

Machi 30
"Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
- Zaburi 37:25

Machi 31
"..Mwambieni, Avaaye asijisifu kama avuaye.
- 1 Wafalme 20:11