Mstari wa Siku

[Copy and send, from here:]

Mstari wa Siku:

Habari za asubuhi! 🙂

https://www.wordproject.org/bibles/votd/index_sw.htm


Mistari ya kila mwezi ya Biblia:


Siku 1
"Kazi yenu ni bure, mnaoamka mapema, Na kukawia kwenda kulala, Na kula chakula cha taabu; Yeye humpa mpenzi wake usingizi.
- Zaburi 127:2


Siku 2
"...Nenda nyuma yangu, Shetani; maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.
- Marko 8:33

Siku 3
"Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.
- Mithali 3:3

Siku 4
"Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.
- 1 Yohana 5:14

Siku 5
"bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
-1 Wakorintho 1:27

Siku 6
"Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.-
- Yohana 3:36

Siku 7
"Jioni, asubuhi, na adhuhuri nitalalama na kuugua, Naye ataisikia sauti yangu.
- Zaburi 55:17

Siku 8
"Maana umekuwa ngome ya maskini, Ngome ya mhitaji katika dhiki yake, Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, Kivuli wakati wa hari; Wakati uvumapo upepo wa watu watishao, Kama dhoruba ipigayo ukuta.
- Isaya 25:4

Siku 9
"Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin, nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.
- Mathayo 17:20

Siku 10
"Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
- Yohana 14:15

Siku 11
"Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieliii naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto.
- Danieli 1:17

Siku 12
"Umngoje Bwana, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje Bwana.
- Zaburi 27:14

Siku 13
"Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
- Yohana 1:1

Siku 14
"Hutaogopa hofu ya usiku, Wala mshale urukao mchana, Wala tauni ipitayo gizani, Wala uele uharibuo adhuhuri,
- Zaburi 91:5,6

Siku 15
"...Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno litathibitishwa.
- 2 Wakorintho 13:1

Siku 16
"Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia.
- Mithali 23:24

Siku 17
"Na chombo kile, alichokuwa akikifinyanga, kilipoharibika mkononi mwake yule mfinyanzi, alikifanyiza tena kuwa chombo kingine, kama alivyoona vema yule mfinyanzi kukifanya.
- Yeremia 18:4

Siku 18
"awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.
- Waefeso 3:16

Siku 19
"Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara, Maana Wewe, Bwana, peke yako, Ndiwe unijaliaye kukaa salama
- Zaburi 4:8

Siku 20
"Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.
- 1 Wakorintho 3:10

Siku 21
"Azibaye masikio yake asisikie kilio cha maskini, Yeye naye atalia, lakini hatasikiwa.
- Mithali 21:13

Siku 22
"Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.
- Zaburi 30:5

Siku 23
"Kisha akawaambia, Enendeni zenu, mle kilichonona, na kunywa kilicho kitamu, tena mpelekeeni sehemu yeye asiyewekewa kitu; maana siku hii ni takatifu kwa Bwana wetu; wala msihuzunike; kwa kuwa furaha ya Bwana ni nguvu zenu.
- Nehemia 8:10

Siku 24
"Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
- Mwanzo 1:26

Siku 25
"Bwana ataniokoa na kila neno baya, na kunihifadhi hata nifike ufalme wake wa mbinguni. Utukufu una Yeye milele na milele. Amina.
- 2 Timothy 4:18

Siku 26
"lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
- 2 Wakorintho 4:2

Siku 27
"Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
- Mithali 3:5,6

Siku 28
"Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
- Waefeso 5:3

Siku 29
"Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
- Luka 1:45

Siku 30
"Tazama, wana ndio urithi wa Bwana, Uzao wa tumbo ni thawabu.
- Zaburi 127:3