Furaha
- Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga daima kelele za furaha. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
 Zaburi 5:11
- 
Utanijulisha njia ya uzima; Mbele za uso wako ziko furaha tele; Na katika mkono wako wa kuume Mna mema ya milele.
 Zaburi 16:11
- 
Maana ghadhabu zake ni za kitambo kidogo, Katika radhi yake mna uhai. Huenda kilio huja kukaa usiku, Lakini asubuhi huwa furaha.
 Zaburi 30:5
- 
Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha.
 Zaburi 126:5
- 
Heri kila mtu amchaye Bwana, Aendaye katika njia yake.   Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.
 Zaburi 128:1, 2
- 
Na hao waliokombolewa na Bwana watarudi, watafika Sayuni wakiimba; na furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao; nao watapata kicheko na furaha, huzuni na kuugua zitakimbia.
 Isaya 35:10
- 
Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.
 Yohana 15:11
- 
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
 Warumi 14:17