Mstari wa Siku

[Copy and send, from here:]

Mstari wa Siku:

Habari za asubuhi! 🙂

https://www.wordproject.org/bibles/votd2/index_sw.htm


Mistari ya kila mwezi ya Biblia:

Jan. 1
"Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani.
- Isaya 43:19

Jan. 2
"Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
- 2 Wakorintho 5:17

Jan. 3
"Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
- Isaya 55:9

Jan. 4
"Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyonitaithibitisha njia yangu mbele yake.
- Ayubu 13:15

Jan. 5
"Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
- Mathayo 7:12

Jan. 6
"Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.
- Waebrania 11:3

Jan. 7
"Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
- Zaburi 119:11

Jan. 8
"Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
- 1 Yohana 4:8

Jan. 9
"Bwana ndiye mchungaji wangu, Sitapungukiwa na kitu.
- Zaburi 23:1

Jan. 10
"Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana.
- Mambo ya Walawi 19:18

Jan. 11
" Lakini yeye aijua njia niendeayo; Akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu.
- Ayubu 23:10

Jan. 12
"Kwa maana maskini hawatakoma katika nchi milele; ndipo ninakuamuru na kukuambia, Mfumbulie kwa kweli mkono wako nduguyo, mhitaji wako, maskini wako, katika nchi yako.
- Kumbukumbu la Torati 15:11

Jan. 13
"akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.
- Kutoka 15:26

Jan. 14
"Kwa sababu hii zitendeni amri zangu, mkazishike hukumu zangu, na kuzifanya; nanyi mtakaa katika hiyo nchi salama.
- Mambo ya Walawi 25:18

Jan. 15
"Kwa maana hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi.
- Marko 4:22

Jan. 16
"Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo.
- Yohana 1:17

Jan. 17
"Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
- Mathayo 5:6

Jan. 18
"Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.
- Warumi 8:1

Jan. 19
"Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.
- Mwanzo 1:27

Jan. 20
"Ni nani niliye naye mbinguni, Wala duniani sina cha kupendeza ila Wewe.
- Zaburi 73:25

Jan. 21
"Farasi huwekwa tayari kwa siku ya vita; Lakini Bwana ndiye aletaye wokovu.
- Mithali 21:31

Jan. 22
"Na watoto wako wote watafundishwa na Bwana; na amani ya watoto wako itakuwa nyingi.
- Isaya 54:13

Jan. 23
"Nitamhimidi Bwana kila wakati, Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
- Psalms 34:1

Jan. 24
"akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. -
- Mathayo 18:3

Jan. 25
"(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;
- 2 Wakorintho 10:4-5

Jan. 26
"Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? Bwana ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
- Zaburi 27:1

Jan. 27
"Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
- Yohana 10:10

Jan. 28
"Bwana atawapigania ninyi, nanyi mtanyamaza kimya.
- Kutoka 14:14

Jan. 29
"Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake.
- Mithali 26:17

Jan. 30
"Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.
- Zaburi 19:14

Jan. 31
"Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
- Mathayo 5:11