0:00
0:00

Mlango 25

Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2 Enzi na hofu zi pamoja naye; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3 Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4 Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5 Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake;
6 Siuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!